Ushahidi kuhusu mauaji ya kiholela na kupotea kwa watu nchini Kenya unaashiria matukio haya yanatekelezwa na vyombo vya usalama. Idara ya usalama ingali inashikilia kuwa haihusiki kwa vyovyote vile. Ikiwa maafisa wa usalama hawahusiki, kwa nini hawafanyi uchunguzi ilhali imo ndani ya uwezo wao kufanya hivyo? Sehemu ya Pili ya Kifo cha Mende inaangazia matukio zaidi ya mauaji na kilio cha haki cha familia za wahasiriwa.
Source: Africa Uncensored