Katika Kenya ya sasa, mauaji ya kiholela imekuwa desturi ya maisha. Si nadra kusikia watu wametoweka katika njia za kutatanisha wasipatikane tena. Iwapo watapatikana, basi watakuwa wameuawa. Hili limekuwa likiendelea kwa miaka mingi huku idara ya usalama ikidaiwa kuhusika. Makala Kifo cha Mende yanaangazia baadhi ya mauaji ya kiholela na kutoweka kwa watu nchini Kenya..